Header Ads

RANGI YA CHUNGWA 12

RANGI YA CHUNGWA 12
WRITER: DEOKING PETER
CONTACT: 0673788242
E-Mail: Deokingpeter@gmail.com
PAGE FB: Story Za Deoking

ILIPOISHIA...............
"Dickson? Kwanini umeamua kunifanyia hivi, nikitu gani nilicho kukosea, hizi ndizo ahari tulizo kubaliana, siamini Dickson kama wewe ndiyo wa kunifanyia hivi. Sikuwahi kufikiria kama lingekuja kutokea jambo kama hili. Angely hili ndilo kubaliano letu, kwanini lakini, nauliza kwanini jamani" Ilikuwa ni sauti ya msichana Johar, ambae alikuwa masomoni kwa kipindi kirefu.

Yale maneno yalisikika kwa sauti kubwa, kila mtu aliekuwa pale aliweza kuyasikia lakini hakuna hata mmoja aliekuwa ameelewa yale maneno, kimya kilizidi kutawala huku Johar akizidi kutokwa na machozi na kilio cha wazi wazi. Kila mtu alishangaa kwa kile kitendo, kwa jinsi Johar alivyokuwa akilia kwa uchungu iliwadhihirishia watu wengi kuwa kulikuwa na tatizo limemsibu msichana huyo. Hakuna alietambua nini kilichokuwa kinamsibu msichana huyo zaidi ya Dickson pamoja na Angely.

ENDELEA.......................
Hali ya ukimya iliendelea kutawala, huku kila mmoja akitamani kujua nini kimetokea hadi hali kama ile kutokea. Watu wengine waliweza kusimama ili kutizama vizuri, hali ile ilikuwa kama filamu, lakini hakukuwa na filamu wala igizo pale, kwa jinsi Johar alivyokuwa akilia kwa uchungu ndipo watu walivyogundua kuwa lile jambo halikuwa na utani. Baba yake Angely alisimama kwa hasira ilikujua nini kimetokea, aliponyanyuka alijikuta anarejea kwenye kiti chake taratibu na kukaa kimya. Ni baada ya kumuona Johar pale mbele, haikujulikana ni kwanini mzee uyo alipomuona Johar alikaa kimya na kutamani kuondoka mahali pale.

"Johar naomba unisamehe, shetani tu ndiyo alinipitia, sikudhamiria kukufanyia hivi, Naomba unisamehe. usiponisamehe nitakuwa mgeni wa nani mimi" Yalikuwa ni maneno ya msichana Angely huku akiwa amepiga magoti mbele ya umati mkubwa kama ule, kila aliekuwa pale alishangaa, wengine waliweka mikono yao kichwani kwa kitendo kile. Angely alikuwa ni bibi harusi mtarajiwa na zilikuwa zimebaki dakika chache kutawazwa kuwa mke halali wa Dickson.

Lile jambo lilimshangaza hata Dickson, yale maneno aliokuwa ameyatamka Angely yalimfanya Dickson kubaki akiwa anamwangalia Angely alivyokuwa analia. Johar hakumjibu chochote alichoamua ni kupiga hatua za haraka haraka kuelekea nje huku machozi yakimtoka kwa wingi, Dickson alivyoona vile aliamua kumkimbilia Johar ili ikiwezekana kumtuliza maana alionekana kuwa na hasira sana, lakini alikuwa amechelewa maana Johar alipofika nje aliingia kwenye gari na kuondoka. Hali ya kule ukumbini ilikuwa imebadilika, hakukuwa na harusi tena.

Kila mmoja alikuwa akizungumza lake, Angely alibaki pale mbele huku akitokwa na machozi, alimsubiri na kuwaza pengine Dickson angerudi lakini haikuwa hivyo. Dickson alipoona Johar kaondoka akiwa na hasira na machozi yakimtoka, alitambua pengine Johar angeweza kufanya kitu kibaya. Aliamua kuingia kwenye gari ili ikiwezekana kumzuia Johar asifanye alichokuwa anataka kukifanya. Mwendo wa gari wa Dickson ulikuwa kasi sana, hiyo yote ni kwaajili ya kumuwahi Johar, Akiwa kwenye gari alikuwa akikumbuka mambo aliokuwa ameyafanya na Johar kipindi cha nyuma, machozi yalianza kumtoka pale alipokumbuka ahadi walizopeana kipindi Johar alivyokuwa anaondoka, alijihisi mwenye makosa.

Akiwa kwenye Dimbwi la mawazo juu ya Johar huku speed ya gari ikiwa ni kali alijikuta anaingia upande wa pili wa barabara na kukuta anasababisha ajali mbaya ya gari. Kutokana na mshituko alijikuta anakanyaga mafuta badala ya breki na hapo ndipo alipolivaa lori la mchanga, kwa vile gari la Dickson lilikuwa Dogo liliweza kubinuka vibaya na kubiringita. Ilikuwa ni ajali mbaya sana, kila aliekuwa karibu na yale maeneo aliweka mikono yake kichwani.

Hazikupita hata dakika tatu, watu walikuwa tayari wamekwisha kujaa eneo la tukio, walipofika ndipo walipomkuta Dickson akiwa anavuja damu sehemu za kichwani, kwa jinsi gari lilivyopinduka liliweza kumsababishia Dickson kupoteza fahamu. Wasamaria wema kwenye lile eneo waliweza kumsaidia kumtoa Dickson katika gari lake, hakuna alietambua ya kuwa Dickson ni mzima aua amekufa. Msaada wa wale watu uliweza kufanya Dickson kufikishwa hospital na kupokelewa na madokta, hali yake ilionekana kuwa mbaya sana.

Hata Dokta alionekana kuweka mikono yake kichwani baada ya kuona mwili wa Dickson, Jitihada za Madokta zilionekana kugonga mwamba, kila walipokuwa wakijaribu kwa kila njia ili hali ya Dickson irudi kama apo awali lakini ilishindikana. taarifa zilifika wa wazazi wa Dickson ambao kwa wakati huo walikuwa wakiwaza kile kilichotokea kwenye harusi ya mtoto wao, lilikuwa ni jambo la aibu sana, waliatokea kumchukia sana Johar na kuhisi bila yeye mtoto wao asingeweza kupatwa na ile ajali.

Kilio kilitwala kwenye nyumba ya Dickson, kila siku walikuwa wakimuomba mungu mtotowao awe salama huku wakiapia na kujisemea kama mtoto wao angelipoteza maisha wangeweza kumuuwa Johar, Kwa wakati huo hakuna aligundua Johar alikuwa wapi. Taarifa zilienea karibu kila redio pamoja na tv ukiachia mbali na magazeti pia. wazazi wa Dickson alifanikiwa kupata zile taarifa kutoka kwenye televisheni/runinga, zilikuwa ni taarifa za kushitua na kuwafanya wajiulize maswali mengi.
ITAENDELEA...................
Picha za mandhari zimetolewa na i-bob. Inaendeshwa na Blogger.