Airtel Fursa yamwaga milioni 10 kwa mjasiliamali kuokoa Mazingira
Mjasiliamali Amina Iddi (20) (kulia ) akijaribu moja ya vifaa
alivyokabidhiwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa wa
kuwezesha vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 24 akizungusha mashine ya
kutengenezea majiko sanifu baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo vyenye
thamani ya sh10 Mil kijijini kwao Magole mtaa wa Chabwanga wilaya ya
Kilosa mkoani Morogoro jana.
Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi akionyesha moja ya jiko
sanifu ambalo bado halijakamili yanayoandaliwa na mjasiliamali Amina
Iddi (20)wa tatu kulia baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wake
wa Airtel Fursa katika hafla iliyofanyika nyumbani kwao katika kijiji
cha Magole mtaa wa Chabwanga wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro