RANGI YA CHUNGWA 5
RANGI YA CHUNGWA 5
WRITER: DEOKING PETER
CONTACT: 0673788242
E-Mail: Deokingpeter@gmail.com
PAGE FB: Story Za Deoking
ILIPOISHIA...............
Aliamua kuondoka na kwenda ofisini kwa bosi wake kwaajili ya kutaka kujua sababu ya yeye kuamishwa bila taarifa, kwa muondoko aliondoka nao Dickson ulikuwa si wakawaida, alionekana kuwa na hasira kwa kile kilichotoke.
Alipofika ofisini kwa bosi wake alizuiliwa kuingia ikiwa tofauti na siku zote alizokuwa akiingia bila kizuizi, aliwaangalia wale watu na kuhisi wamechanganyikiwa, aliwaamuru wampishe lakini hakuna aliemsikiliza zaidi ya kusukumwa na kutolewa hadi nje ya geti la kuingilia. Kwa bahati nzuri bosi wake ndiyo alikuwa anaingia, Dickson hakufanikiwa kumuona bosi wake lakini bosi wake alifanikiwa kumuona na kushuka kwenye gari na kusogea mahali alipokuwa Dickson.
ENDELEA.................
Dickson alishindwa kuelewa kwanini alikuwa anazuiliwa kuingia kwenye ofisi ya bosi wake, akiwa anataka kuondoka alishangaa kumuona bosi wake mbele yake, alishtuka maana hakutegemea kitu kama kile, kilikuwa kitu cha kushtukiza na kumfanya Dickson kushtuka. Dickson alishindwa kuongea na kuona mdomo wake kuwa mzito kutamka kile alichotaka kumwambia bosi wake ofisini kwake.
"Dickson mbona upo hapa sasa hizi, wakati huu ni muda wa kazi?"
Aliongea bosi wake na kumfanya Dickson kutumbua macho kama mtu aliekanyaga nyoka, kiukweli lile swali lilikuwa kama mtego kwake, maana muda siyo mrefu alipokea barua kutoka kwa Mtoto wa bosi huyo kuwa ameamishwa kikazi na ameamishiwa Jijini Dar es salaam.
"Mbona unaonekana kama mtu anae ekti jambo flani. Unajua Dickson wewe ni kama mwanangu ila huko unapoelekea siko, utakuja kujikuta unaharibu maisha yako kwa mtu asiekuwa na thamani kwako. Kuna muda wa kazi na muda wa mapenzi, embu jiangalie ulivyobadilika hadi nakuhurumia, laiti ningalimjua huyo msichana anaekufanya unakuwa katika hali kama hii sijui nini kingetokea"
Aliongea bosi wake na Dickson ambae alikuwa ni kama Baba kwake, Dickson alibaki mdomo wazi kama ilivyo kawaida yake pale anapoulizwa swali la kumshangaza, au kitu chochote cha kustaajabisha. Dickson alishndwa kuelewa zile taarifa bisi wake amezipata wapi maana muda mwingi Bosi wake huwa ofisini kwake na wakati mwingine huwa kwenye safari mbali mbali za kikazi, alihisi huenda bosi wake alikuwa akimfuatilia kwa kipindi kirefu, ndiyo maana akawa analitambua lile jambo.
"Kama alikuwa ananifutilia mbona anaonekana hamtambui msichana huyo au kaambiwa na mtu"
Dickson alijikuta anazungumza maneno ya chini chini bila kujua sauti yake ilisikika vizuri katika masikio ya bosi wake.
"Nadhani nikija ofisini kwako tutaonge mengi, cha muhimu nakutakia safari njema"
Aliongea bosi wake kwa ufupi na kumkumbatia Dickson, kiukweli bosi huyo alionekana kuto ridhika kwa kuondoka kwa Dickson na kuonekana kumpenda na kumthamini kama mwanae.
Bosi wake ambae alijulikana kwa jina la Visent alimuacha Dicksoni pale na kuondoka kuelekea ndani ya ofisi yake.
Dickson alirudi nyumbani akiwa hana furaha kabisa, alipofika alishangaa na mazingira aliyo yakuta, nyumba ilikuwa tofauti na siku zote, ilionekana kusafishwa vizuri na kupangwa vizuri. Kilikuwa kitu cha kushangaza maana alijua mpenzi wake hakuwa nanafanya usafi hivyo aliamini siyo mpenzi wake aliefanya ule usafi.
Kila kitu kilikuwa kimepangwa kwa utaratibu maalumu, akiwa sebleni alishangaa kumuona mpenzi wake akiwa anatokea chumbani akiwa amependeza sana, tofauti na siku za nyuma, alihisi yupo kwenye ndoto. Lakini haikuwa ndoto bali ilikuwa ni kweli kwa kile alichokuwa anakiona. Alimwangalia mpenzi wake mara mbili mbili kwa jinsi alivyoongezeka uzuri wake na kuwa kama malaika.
Mpenzi wake alimkaribisha vizuri huku mezani kukiwa kumeandaliwa vizuri, kila kitu kilikuwa tofauti na siku zote, kitu ambacho kilimfanya Dickson kushangaa, hakuwai kuona kitu kama kile tokea ameanza kuwa na mpenzi wake, japo alikuwa hana furaha kutokana na kuamishwa kikazi na kuhisi atamuacha mpenzi wake, likini alijisikia furaha baada kuonana na mpenzi wake.
"Johar mpenzi upo tayari kwenda na mimi Dae es salaam?"
Aliuliza Dickson huku akiwa anamwangalia mpenzi wake kwa jicho la huzuni.
ITAENDELEA............