Header Ads

RANGI YA CHUNGWA 9

RANGI YA CHUNGWA 9
WRITER: DEOKING PETER
CONTACT: 0673788242
E-Mail: Deokingpeter@gmail.com
PAGE FB: Story Za Deoking

ILIPOISHIA...............
Kichwa chake kilitawaliwa na mawazo mengi, akili yake haikuwaza jambo lingine zaidi ya kwenda kuozea jela. Akiwa pale alishangaa na kutamani kukimbia baada ya kuwaona polisi wakizunguka maeneo yale, akiwa katika mshangao mkubwa alishtukia pingu zikiwa zinaingia katika mikono yake na kujikuta amekamtwa na polisi bila kujua hatima ya yote. Kilikuwa ni kitu cha kushtukiza, hakukuwa na maelezo yoyote.

Rafiki yake na Angely alionekana kutoshtuka kwa kitendo cha kukamatwa kwa Dickson, ilionyesha dhahiri msichana huyo yeye ndiye alietoa taarifa hizo kwa polisi. Dickson alichukuliwa kwa nguvu huku akiwa anajiuliza maswali mengi kichwani kwake, mwili wake ulionyesha kutetemeka na jasho lilizidi kumtoka. Alipakiwa kwenye gari la polisi na kufikishwa kituo cha polisi, kitendo cha kufika kituo cha polisi alipokelewa na kipigo kikali. Ndani ya muda mfupi nguo zake zilikuwa zimelowa damu, kila kona ya mwili wake kulikuwa na maumivu.

ENDELEA.....................
Nyumbani kwa kina Dickson waliandaa vitu vizuri kwaajili ya kumkaribisha mtoto wao ambae ni muda mrefu walikuwa hawajaonana. Familia hiyo ilimpenda kijana wao kupita maelezo, taarifa za mtoto wao kuamishwa kikazi walizifahamu vilivyo maana wao ni moja ya watu waliochangia, mtoto wao kuamishwa. Walijua mtoto wao angeliwahi kufika maana tiketi aliokatiwa ilikuwa ni ya gari za alfajiri, walimsubiri kwa hamu kubwa huku wakiandaa vitu kemkemu kwaajili ya kijana wao.

Masaa yalisogea na kusogea hadi ikawa imefika saa kumi na moja hawakuwa wamemuona kijana wao, walijipa moyo wakihisi pengine gari ndilo lililochelewa kufika. Hadi inafika saa moja usiku bado Dickson hakuonekana, wasiwasi uliwashika wazazi hao hofu iliwashika, ndipo walipoamua kupiga simu kwa gari ambalo alitakiwa kuja nalo kijana wao.

Taarifa walizozipata ziliwashtua sana maana waliambiwa gazi walilokuwa wanalizungumzia lilikuwa jijini hapo toka saa kumi. Zile taarifa ziliwapa mawazo mengi na kujiuliza mtoto wao amepatwa na nini, kimya kilitawala katika nyumba hiyo. Tukija kwa upande wa Dickson hali yake ilikuwa mbaya, kipigo alicho kuwa amekipata kutoka kwa polisi kilimfanya mwili wake kujawa na maumivu makali. Alishindwa kuelewa ni kwanini alikuwa akipigwa namna ile, alijihisi mtu asiekuwa na hatia, alifungiwa kwenye moja ya vyumba ambavyo wengi tunapenda kuita lokapu.

Siku zima kijana alikuwa ndani ya chumba hicho huku akiwa na maumivu makali, hakuna hata mmoja aliekuwa anatambua kilichokuwa kimempata Dickson, wazazi wake walibaki na maswali mengi hata bosi wake alishindwa kuelewa kilichomkuta Dickson. Walijaribu kwenda nyumbani kwa Dickson kumwangalia lakini hakuna walichofanikiwa zaidi ya kukuta vitu vyake vya kusafiria, hali ya kumtafuta Dickson iligonga mwamba. Mateso yaliendelea kwa Dickson kila siku, chakula kwake ilikuwa ni gumnz. Hakufanikiwa kujua kama Angely amepona au la, alibaki mwenye mawazo mengi.

Akiwa pale kituoni aliweza kupata ugeni, ugeni ule ulimfanya Dickson kuona Mungu amejibu maombi yake,ambayo alikuwa akiomba kila kukicha.
"Habari yako kijana?"
Alisalimiwa baada ya kuketi kwenye kiti, alipomwangalia yule mtu alionekana kumfahamu lakini hakukumbuka alikwisha muona wapi.
"Nzuri tu kaka"

Alijibu kiunyonge na kuonekana kama mtu aliekata tamaa.
"Nadhani unanikumbuka vema, ila kumbukumbu zako zisikufanye kuona nimekuja kukupa msaada. Kwa kitendo ulichokifanya hakika lazima ufie jela. Aliongea mtu huyo na kumfanya Dickson kukaa kimya kutafakari yale maneno aliyokuwa ameambiwa, alikumbuka yule mzee alikuwa ni nani. Alipokumbuka kuwa yule mzee ni moja ya wateja wake ambao alikuwa anawasaidia katika kesi zao mbali mbali alishangaa sana.

Yale maneno yalimuweka kwenye wakati mgumu kmna kujiuliza kipi kibaya alichokifanya, kauli ya yule mzee ikimfanya Dickson kuwa kwenye hali ya sintofahamu.
"Yaani wewe mtoto wa malaya unaweza kunipigia mwanangu kiasi kile, mimi mwenyewe unae niona hapa siwezi kumfanyia mtoto wangu au kumpiga kiasi kile. Sasa kaa ukijua endapo mwanangu atapatwa na tatizo lolote jua wewe utawajibika kwa yote, mpuuzi mkubwa wewe" Aliongea mzee huyo, maneno yaliozidi kumfanya Dickson kuchanganyikiwa.

Yalikiwa ni maneno yaliojawa na hasira pamona jaziba nyingi, Dickson alitaka kuzungumza kitu lakini mzee huyo hakuwa tayari hata kidogo, hakutaka kusikia hata sauti ya kijana Dickson. Baada ya kuondoka mzee huyo Afande alimchukua Dickson na kumrudisha ndani, maisha ya Dickson yalikuwa kwenye wakati mgumu sana.

"Inawezekana yule ndiye Baba yake na Angely? Hapana! Inawezekanaje, mbona huyo mzee ni tajiri sana iweje mtoto wake awe kwenye maisha kama yale ya kiswahilini" Alijiuliza Dickson huku akijaribu kujiuliza juu ya Angely, hakukuwa na mtu wa kumjibu maswali yake, machozi yalianza kumtika huku akikimbuka vitisho vya mzee alie semekana kuwa Baba wa Angely.

Taratibu alianza kuwakumbuka wazazi wake, alijutia sana kwa kuwasaliti wazazi wake kwa muda mrefu. Hakuwa na uwezo wa kuwapa taarifa wazazi wake, hali ya pale polisi ilikuwa mbaya, njaa ilimyesa maana chakula alikipata kwa shida. Manyanyaso yalitosha kabisa kumkondesha, siku nne zilipita bila kuwa na msaada wowote au taarifa yoyote kuhusu Angely au wazazi wake, alihisi mambo yale yote na ndoto zake zote zingeishia gerezani.

Alianza kuona Angely ndiye mkombozi wake, alijua endapo Angely angepona basi na yeye angekuwa salama, maombi yake yote yalikuwa juu ya msichana huyo.
"Kijana vipi unayaonaje haya maisha, sizani kama kuna uwezekano wa wewe kutoka humu. Nataka nikuambiekuwa usije ukafikiria kama kuna atakae kuja kukutoa huku, labda nikuulize swali dogo tu. Kwanza uliingiaje ndani kwa mtoto wangu mtu kama wewe, inaonyesha kabisa ulikwenda kwa lengo la kumbaka alivyo kataa ndiyo ukaamua kumpiga na kumuumiza kiasi kile" Ni maneno ya luomfanya Dickson kunyanyuka pale chini alipokuwa amelala na kukuta ni yule mzee, aliesemekana ni Baba wa Angely. Yale maneno yalimshitua sana Dickson na kumfanya ashindwe kuelewa yule mzee alikuwa anamaanisha nini, hakika yalikuwa ni maneno ya kushtusha.

"Mimi nimebaka, nime mbaka nani mimi, naomba unielewe Baba yangu mimi sijabaka na wala sikutaka kumbaka mwanao, kweli kabisa hata yeye mwenyewe kama angelikuwa hapa asinge kubaliana na maneno yako"
Aliongea kijana huyo kujitetea kwa mzee huyo, lakini mzee huyo hakutaka kabisa kumsikiliza Dickson wala kumuelewa. Mzee huyo alieonekana kuwa na fedha nyingi ni kwa muonekano wake alivyokuwa, alionekana kutokuwa na roho ya huruma hata kidogo.
ITAENDELEA....................

Picha za mandhari zimetolewa na i-bob. Inaendeshwa na Blogger.