Header Ads

RANGI YA CHUNGWA 8

RANGI YA CHUNGWA 8
WRITER: DEOKING PETER
CONTACT: 0673788242
E-Mail: Deokingpeter@gmail.com
PAGE FB: Story Za Deoking

ILIPOISHIA...............
Yalikuwa ni maombi ya kijana huyo ambae alikuwa na zaidi ya miezi sita hakuwa anajua kanisa wala hakumkumbuka Mungu zaidi ya kula raha na mpenzi wake, machozi yalimtoka huku akiwa afanya maombi ya kumlinda mpenzi wake. Kiukweli Dickson alimpenda Johar kuliko kitu chochote hapa duniani, alionekana kumjali na kumsamini, hakuwa na utani kabisa na mapenzi yake yeye pamoja na mpenzi wake Johar. Saa zilisogea hadi ilipofika asubuhi Dickson hakupata usingizi kabisa, saa moja asubuhi Dickson alikuwa mlangoni kwa rafiki yake Johar, alipofika aligonga kwa muda bila mafanikio, alivyojaribu kuzungusha kitasa cha mlango huo alijuta mlango haujafungwa. Aliamua kuingia ndani ya chumba cha msichana huyo aliejulikana kwa jina la Angely, alipoingia alishtuka na kuahangaa maana alimkuta Angely akiwa kama alivyozakiwa.

ENDELEA...........
Ile hali ilimfanya Dickson kushtuka na kuhisi amefanya makosa kuingia chumbani kwa msichana huyo bila idhini yake, alibaki akiwa anajiuliza kuingia ndani au kutoka nje, ile hali ilimfanya abaki ameduwaa asijue nini cha kufanya. Wakati akiwa kwenye hali ya kutafakari alishtukia anavutwa mkono wake na msichana huyo, kilikuwa ni kitu cha kushtukiza na kujikuta anaingia ndani bila kupenda. Alishindwa kujizuia na kujikuta ameangukia kwenye kifua cha msichana huyo, alipotaka kujinyanyua alijikuta anashindwa maana msichana huyo alikuwa amemshika na kumtaiti vilivyo, ile gali ilimfanya Dickson kushangaa na kushindwa kuelewa alichokuwa anakihitaji msichana huyo. Taratibu msichana huyo alianza kumpapasa Dickson huku akijaribu kuonyesha hisia zake kwa kijana, hakikuwa kitu cha masihara maana yote aliokuwa anayafanya msichana huyo alikuwa akifanya kwa kumaanisha. Dickson alimuheshimu msichana huyo maana alikuwa ni rafiki wa mpenzi wake, ilimuwia ngumu kufanya mapenzi na msichana huyo aliejulikana kwa jina Angely.

"Angely embu acha ujinga unaotaka kuufanya"
Aliongea Dickson huku akiobekana kukasirishwa na lile jambo, lakini msichana huyo hakutaka kusikiliza maneno ya Dickson, aliendelea kufanya alichokuwa anakifanya. Hasira zilimshika kijana huyo na kumsukuma kwa nguvu msichana huyo, kile kitendo cha kumsukuma msichana huyo na kuanguka chini kilimshtua sana. Msichana Angely alipoanguka chini alijikuta anaangukiwa kichwa na kujipigiza chini, damu zilitapakaa pale ndani. Dickson alikuwa kama mtu aliegandishwa, baada ya kuona damu zikiwa zimetapakaa huku Angely akiwa amelala chini na kuwa kimya alishtuka sana. Kimya kilitawala huku taratibu machozi yakiwa yanamtoka kijana Dickson, alihisi ameuwa alimsogelea Angely na kumuita bila mafanikio.

Hakuweza kwa kile kilichotokea, katika maisha yake hakuwahi kufikiria jambo kama lile lingeweza kumtokea. Alihisi joto angali kulikuwa baridi, mapigo ya moyo wake yaliongezeka kasi, mwili wake ulionekana kutokwa na jasho jingi hata nguo alizokuwa amevaa zilionekana kulowa kwa chasho. Hofu ilimjaa, alihisi kuishiwa nguvu. Alianza kujilaumu kwanini alifika pale, hakutaka kitu kama kile kitokee. "Angely shosti leo mbona umelala sana vipi leo huendi kazini?" Nisauti ya rafiki wa karibu na msichana huyo, mtu ambae walikuwa wanakaa nae kwenye ile nyumba japo vyumba vyao vilikuwa tofauti. Ile sauti ilimfanya kijana Dickson kushtuka na kuanza kutetemeka kwa hofu akihisi segerea panamuita.

Kwa vile mlango ulikuwa wazi aliamua kutembea kwa kunyata kwenda kuufunga ili rafiki yake na Angely asiweze kujua kilichokuwa kinaendelea, Dickson aliamini kama msichana huyo angegundua kilichotokea basi alijua lazima angeozea segerea. Alipofika mlangoni akiwa tayari kufunga mlango huo alishtukia mlango unafunguliwa na kuingia msicha aliekuwa rafiki wa Angely, kile kitendo cha msichana huyo kuingia ndani na kumkuta Dickson huku rafiki yake kipenzi akiwa amelala chini huku akizidi kutokwa na damu nyingi tena akiwa kama alivyo zaliwa, binti huyo alionyesha mshituko mkubwa. Lilikuwa nu jambo la kushtukiza maana hakutegemea kitu kama kile.

Dickson alizidi kuchanganyikiwa baada ya kuingia kwa rafiki wa Angely, kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa, yule msichana alimsogelea Angely akiwa anaogopa hata kumgusa kwa jinsi alivyokuwa ameumia na kutoka damu nyingi, alipomfika na kumgusa aligundua Angely alikuwa mzima, alionekana kulitambua hilo mapema na kumwambia Dickson wasaidiane kumpeleka hospital. Kijana Dickson hakutaka kupoteza muda, alimyanyua Angely na kuanza kutoka nae nje ya chumba chake, walitembea mwendo wa haraka kwa kutaka kuwahi ili ikiwezekana kuokoa maisha ya msichana huyo. Maombi ya kila aina yalipita katika kinywa cha Dickson huku akiapiza kwa kila aina na kutoa ahadi ambazo hakutambua alichokuwa akikisema. Kiukweli Dickson alionekana kuchamyikiwa.

Baada ya muda kidogo walifanikiwa kufika katika hospital ambayo ilikuwa karibu na maeneo yale, walipofika walipokelewa na Angely alichukuliwa na kupelekwa katika vyumba vya wagonjwa mahuti huti, shati la kijana huyo lilibadilika na kuwa jekundu kutokana na damu zilivyokuwa zilivyo mlowanisha. Kichwa chake kilitawaliwa na mawazo mengi, akili yake haikuwaza jambo lingine zaidi ya kwenda kuozea jela. Akiwa pale alishangaa na kutamani kukimbia baada ya kuwaona polisi wakizunguka maeneo yale, akiwa katika mshangao mkubwa alishtukia pingu zikiwa zinaingia katika mikono yake na kujikuta amekamtwa na polisi bila kujua hatima ya yote. Kilikuwa ni kitu cha kushtukiza, hakukuwa na maelezo yoyote.

Rafiki yake na Angely alionekana kutoshtuka kwa kitendo cha kukamatwa kwa Dickson, ilionyesha dhahiri msichana huyo yeye ndiye alietoa taarifa hizo kwa polisi. Dickson alichukuliwa kwa nguvu huku akiwa anajiuliza maswali mengi kichwani kwake, mwili wake ulionyesha kutetemeka na jasho lilizidi kumtoka. Alipakiwa kwenye gari la polisi na kufikishwa kituo cha polisi, kitendo cha kufika kituo cha polisi alipokelewa na kipigo kikali. Ndani ya muda mfupi nguo zake zilikuwa zimelowa damu, kila kona ya mwili wake kulikuwa na maumivu. ITAENDELEA...................

Picha za mandhari zimetolewa na i-bob. Inaendeshwa na Blogger.