Header Ads

RANGI YA CHUNGWA 10

RANGI YA CHUNGWA 10
WRITER: DEOKING PETER
CONTACT: 0673788242
E-Mail: Deokingpeter@gmail.com
PAGE FB: Story Za Deoking

ILIPOISHIA...............
Kichwa chake kilitawaliwa na mawazo mengi, akili yake haikuwaza jambo lingine zaidi ya kwenda kuozea jela. Akiwa pale alishangaa na kutamani kukimbia baada ya kuwaona polisi wakizunguka maeneo yale, akiwa katika mshangao mkubwa alishtukia pingu zikiwa zinaingia katika mikono yake na kujikuta amekamtwa na polisi bila kujua hatima ya yote. Kilikuwa ni kitu cha kushtukiza, hakukuwa na maelezo yoyote.

Rafiki yake na Angely alionekana kutoshtuka kwa kitendo cha kukamatwa kwa Dickson, ilionyesha dhahiri msichana huyo yeye ndiye alietoa taarifa hizo kwa polisi. Dickson alichukuliwa kwa nguvu huku akiwa anajiuliza maswali mengi kichwani kwake, mwili wake ulionyesha kutetemeka na jasho lilizidi kumtoka. Alipakiwa kwenye gari la polisi na kufikishwa kituo cha polisi, kitendo cha kufika kituo cha polisi alipokelewa na kipigo kikali. Ndani ya muda mfupi nguo zake zilikuwa zimelowa damu, kila kona ya mwili wake kulikuwa na maumivu.

ENDELEA..........................
Dickson alibaki akimuomba Mungu huku akiamini lazima kwenda jela, mtu pekee aliekuwa akimuwaza kwenye akili yake na kuamini ni ndiye msaada wake na mkombozi wake ni msichana Angely, aliamini yeye ndiye mwenye uwezo wa kutoa pale alipokuwa, kwakuwa yeye ndiye anajua ukweli juu ya kile kilichotokea.
"Dickson Michael, umri wa miaka 25 unatuhumiwa na kesi mbili, huku kila kesi ikiwa na sheria zake na adhabu zake. Hivyo kama mahakama imeamua kukupa adhabu ya kwenda jela miaka sit....
"Hapana, hapana nasema, hausiki hata kidogo, msimuhukumu kwa kosa lisilo kuwa lake.
Mimi hapa ndiye mwenye makosa"

Nisauti iliowafanya wengi kugeukia upande ile sauti ilipokuwa inatokea, kijana Dickson alipogeuka hakuamini macho yake. Alikuwa ni Angely alikuwa afungwa na kuzungushiwa bandeji katika kichwa chake, kila mtu alionekana kushangazwa na lile jambo. Dickson hakuamini kile alicho kiona, hata hakimu alionekana kuduwaa na kukosa la kusema. Hali ya pale ndani ilibadilika, Baba yake Angely alikasirika sana kwa kitendo cha mtoto wake kumdhalilisha, maana mzee huyo alidhamitia kumpeleka Dickson jela. Angely alisogea hadi mahali alipokuwa Dickson na kumkumbatia huku machozi yakimtoka, kwa jinsi Angely alivyokuwa ilidhihirisha kuwa alikuwa na hisia kali za kimapenzi kwa Dickson.

"Dickson naomba unisamehe kwa yote yaliotokea, sikutaka iwe vile, nilishindwa kuvumilia Dick. Nakupenda sana Dick. Naongea haya kutoka moyoni mwangu. Nakupenda Dick nipe nafasi katika moyo wako"
Aliongea Angely huku akiwa amemkumbatia Dickson, yale maneno yalikuwa kama utani lakini hakukuwa na utani. Watu wote waliokuwa pale walishangazwa na kile kitendo, aibu iliwajaa kwenye nyuso zao, Baba wa Angely alikasirika sana kwa kitendo kile, lakini Angely hakujali, alichokuwa akikihitaji ni yeye kuwa na Dickson. Baada ya Angely kutoa visibitisho hatimaye Dickson aliachiwa na kuwa huru, japo alikuwa na maumivu makali kutokana na kipigo alichokipata kule kituoni.

Dickson alivyotoka hakutaka zile taarifa zifike kwa wazazi wake wala bosi wake, lakini alikwisha kuchelewa maana taarifa zilikwisha fika kwa wazazi wake, hakuwa na wazo lolote kwa kile kilichotokea, aliamini Angely ndiye aliokoa maisha yake. Aliporejea nyumbani alipokuwa anaishi alishangaa sana kwa jinsi alivyo pakuta, hali ya nyumba yake ilimpa wasiwasi mkubwa. Alibaki amesimama nje huku Angely akiwa pembeni yake, ghafla wakatokea watu wapatao wanne wakiwa wameshikilia chuma zenye mfano wa nondo, Ile hali iliwafanya Dickson pamoja na Angely kushtuka na kutamani kukimbia lakini ilishindikana.

Hawakujua ni kitu gani wamekifanya kibaya hadi kuvamiwa na wale watu, ile hali izidi kumuogopesha Dickson na kuamini ule ungelikuwa mwisho wake, muonekano wa wale watu haukuwa na nia nzuri, ulionekana kutokuwa na nia nzuri. Angely alionekana kuwatambua wale watu, na hata wale watu walipomuona Angely walishtuka na kurudi nyuma hatua kadhaa, lile jambo lilimshangaza Dickson na kujiuliza maswali asipate jibu.
"Najua Baba ndiye kawatuma, ila mwambie endapo Dick ataumia ajue sitomsamehe, bora mniuwe mimi kwanza kabla Dick ajaf.." Kabla hajaendelea liliingia gari la kifahari huku likiwa na milango mitatu kila upande, lilizungushiwa tintedi kila kona, hivyo ilikuwa ngumu kuona kilichokuwa mle ndani, Dickson alibaki akiwa ameduwaa baada ya kumuona Baba yake na Angely ameshuka kwenye lile gari, mapigo ya moyo ya Dickson yalionekana kwenda mbio kitu kilichompelekeaAngely kupeleka mkono wake kifuani kwa Dickson, ile hali ilimuogopesha sana Angely alishindwa kuelewa ni kwanini Dickson alikuwa kwenye hali kama ile.

Dickson alimuogopa sana mzee huyo, ni kutokana na vitisho alivyovipata akiwa kule polisi, alijua mzee yule hakuwa mwema sana kwake. Alipofika pale tulipokuwa tumesimama wale watu walimpa heshima kubwa, kwa jinsi wale watu walivyokuwa wakifanya ilikuwa ni kama muvi "movie" lakini hakuwa na movie. "Dick mpenzi usiogope utakuwa salama, kama ni kufa tutakufa pamoja. Namfahamu vizuri Baba yangu, ila usijali utakuwa salama, ila Dick naomba uniambie unanipenda. Mwenzio sina raha, sitamani kuishi bila wewe" Aliongea msichana huyo maneno ambayo aliyarudia kila saa kwa kijana Dickson, Dickson hakuwa tayari kuamishia mapenzi yake kwa msichana huyo angali alikuwa anajua ana mpenzi aliekwenda masomoni kwa muda. ITAENDELEA.......................

Picha za mandhari zimetolewa na i-bob. Inaendeshwa na Blogger.