RANGI YA CHUNGWA 4
RANGI YA CHUNGWA 4
WIRTER: DEKOKING PETER
CONTACT: 0673788242
E-Mail: Deokingpeter@gmail.com
PAGE FB: Story Za Deoking
ILIPOISHIA.............
"Baba pamoja na Mama yako wametoka muda siyo mrefu, wameelekea kwa shangazi yako"
Aliongea yule sekretar na kunifanya niwaze juu ya yule mtu niliemuona akiwa anafanana na Mama yangu. Dickson alibaki akijiuliza masali mengi kichwani kwake bila kupata jibu kamili, aliamini kile alichokiona alikuwa hajaona vizuri.
Aliendelea na shughuli zake huku mpenzi wake akiwa karibu yake kila wakati. Baba yake na Mama yake waliendelea kuumiza vichwa vyao kutokana na mtoto wao kubadilika hadi kufikia hatua ya kutowafikiria wazazi wake, walizidi kushangazwa na mtoto huyo kwa hali ya maisha aliokuwa anayaishi. Liukweli ilikiwa ni aibu kwa mtu kama Dickson kuishi maisha kama yale. Wazazi wake waliamua kufanya utaratibu wa kumuamisha Dickson pale mkoani ili kuepukana na aibu kutoka kwa msicha yule, maana walihisi yule msichana hakuwa mwema kwa mtoto wao.
ENDELEA.............
Ikiwa ni asubuhi kama ilivyokuwa desturi au taratibu alizojiwekea kijana huyo, alijiandaa vema kwaajili ya kwenda kazini kwake. Wakati akiwa anaondoka nyumbani kama kawaida yake aliwasiliana na mpenzi wake na walikubaliana wangeweza kuonana pindi atakapo toka kazini. Dickson alipofika ofisini kwake alikuta utaratibu umebadilika, alishindwa kuelewa nini kilichokuwa kikiendelea, ofisi yake ilikuwa imebadilishwa huku kukionekana kila kitu kilichokuwamo kwenye ile ofisi si vyake, alizidi kuchanganyikiwa maana vitu vyake vya muhimu havikuwamo ofisini kwake havikuwmo. Wakati akiwa anazidi kukagua na kutafuta baadhi ya vitu vyake.
"Au nimekosea ofisi"
Alijiuliza baada ya kukosa vitu vyake, kiukweli alionekana kuchanganyikiwa, alizunguka huku na huku bila mafanikio. Kwa haraka haraka na kwajinsi alivyokuwa alionekana kuchanganyikiwa.
Alipoona vile aliamua kutoka nje kuangaza kama ni kweli ile ni ofisi yake, alivyotoka na kuangalia aligundua ofisi ni ile ile ya siku zote, alibaki pale nje akiwa anajiuliza maswali mengi, akizidi kujiuliza juu ya mabadiliko ya ofisi yake alishangaa kuona gari aina ya Rav4 nyeusi iliozungukwa na tintedi kila kona, ikiingia na kupaki pembeni ya ofisi hiyo, ndipo aliposhuka mdada mrembo akiwa ameshikilia funguo la gari hilo huku pembeni akiwa na karatasi nyeupe ambazo zilionekana kuwa na maandishi.
Mwana dada huyo alimwangalia Dickson bila ya hata salamu, Dikson kwa haraka haraka alijua yule alikuwa ni mteja, alishindwa kumkaribisha maana aliwaza kuhusu vitu vyake.
"Bila shaka wewe ni Dickson?"
Aliongea msichana huyo baada ya kumfikia Dickson.
"Ndiyo mimi sijui nikusaidie nini?"
Alijibu huku akionekana kutokuwa sawa.
"Vizuri maana nafikiri ujumbe niliopewa umefika"
Aliongea msichana huyo huku akiwa anamkabithi yale makaratasi Dickson, Dickson aliyachuka yale makaratasi na kunza kuyasoma, Alishtuka baada ya kusoma na kumgeukia yule msichana na kubaki akiwa anamshangaa. Ilikuwa ni barua ya kuamishwa kikazi na yule msichana alikuwa ni mtoto wa bosi wake, alibaki akiwa ameduwaa hadi yule msichana akabidi amuullize.
"Vipi Dickson mbona unashangaa hivyo, inaana hizi taarifa hukuwa nazo"
Dickson alitikisa kichwa chake kuashiria hakuwa na zile taarifa, kigugumizi kilimshika ghafla, alishindwa hata kuongea.
"Mbona hizi taarifa kila mtu anazifahamu tena tayari ofisi yako ipo na inakusubiri wewe tu maana vitu vyako vyote vimesha safirishwa na nadhani vitakuwa tayari ndani ya ofisi mpya"
Aliongea msichana huyo ambae na kumfanya Dickson kushtuka kwa zile habari, zile taarifa zilikuwa kama ndoto lakini haikuwa ndoto, zilimwingia akilini ipasavyo hakuwa na uwezo wa kufanya lolote maana alietoa zile taarifa alikuwa ni bosi wake.
Aliamua kuondoka na kwenda ofisini kwa bosi wake kwaajili ya kutaka kujua sababu ya yeye kuamishwa bila taarifa, kwa muondoko aliondoka nao Dickson ulikuwa si wakawaida, alionekana kuwa na hasira kwa kile kilichotoke.
Alipofika ofisini kwa bosi wake alizuiliwa kuingia ikiwa tofauti na siku zote alizokuwa akiingia bila kizuizi, aliwaangalia wale watu na kuhisi wamechanganyikiwa, aliwaamuru wampishe lakini hakuna aliemsikiliza zaidi ya kusukumwa na kutolewa hadi nje ya geti la kuingilia. Kwa bahati nzuri bosi wake ndiyo alikuwa anaingia, Dickson hakufanikiwa kumuona bosi wake lakini bosi wake alifanikiwa kumuona na kushuka kwenye gari na kusogea mahali alipokuwa Dickson.
ITAENDELEA...............