Header Ads

RANGI YA CHUNGWA 1

RANGI YA CHUNGWA 1
WRITER: DEOKING PETER
CONTACT: 0673788242
E-mail: Deokingpeter@gmail.com
FB PAGE: Story Za Deoking
Ni kijana mwenye akili nyingi za kufikiria na kutatua jambo, katika maisha yake hakuwahi kufanya jambo likawa baya mbele za watu. Mungu alimjalia kwa kumpatia wazazi bora wenyekujua majukumu yao, walimjali mtoto huyo ambae alikuwa wa pekee katika familia hiyo, alipata elimu bora hadi kufikia kuwa mtu mkubwa serikalini.

Kazi alioipenda alipenda kuwa hakimu, kitu ambacho hapo awali wazazi wake walikikataa ila kwa kuwa kijana huyo alikuwa na ndoto hizo hawakuwa na namna zaidi ya kukubaliana nae. Kwavile wazazi wake hawakutaka kukaa mbali na mwanao waliamua kumshawishi abaki jajini Dar es salaam ili kuwa karibu na wazi wake, lakini kijana huyo alitaka afanyie kazi zake mkoa Arusha, akiamini hali ya hewa na mazingira ya mkoa huo yangalimfaa.
Wazazi wake hawakuwa na kipingamizi wa walikubaliana nae maana walimpenda sana na kumjali. Kijana huyo alianza kazi mkoani huko akiwa anawasilia na wazazi wake zaidi ya mara mbili kwa siku. Ilipita miezi kadhaa mawasiliano yakaanza kuwa hadimu, ilikuwa asipotafutwa na wazazi wake basi yeye hakushuhulika nao, akiwa mkoani huko alifanikiwa kupata mpenzi ambae alifanikiwa kuuteka moyo wa kijana huyo. Alimjali msichana huyo kuliko kitu chochote, hata kazi aliokuwa nayo aliiona haina thamani kama angelikaa mbali na msichana huyo.
Hakufikiria kama anafamilia alichokijali na kukijua katika akili yake ni Msichana huyo aliejulikana kama Johari, msichana mwenye asili ya kimbulu. Kiukweli kama wanavyosema mapenzi ni ugonjwa basi kwa kijana Dockson ilikuwa ni zaidi ya ugonjwa, naweza kusema ilikuwa kama ulimbukeni wa mapenzi, ni kwajinsi kijana huyo alivyo jitoa kwa mwanadada huyo bila kufikiria.
Familia ya Kijana Dickson ilishindwa kuelewa kilicho mpata mtoto wao kuwa kimya kwa kipindi chote, bila hata kuwatafuta wazazi wake, waliwaza ambo mengi katika vichwa vyao bila kupata jibu kamili. Waliamua kufunga safari kuelekea mkoani ambapo mtoto wao alikuwa akifanya kazi, walikubaliana kwa pamoja kwenda kumuona mwanao bila taarifa, kwa lugha nyingine waliamua kumfanyia "suprice".
Asubuhi na mapema wazazi hao walikuwa maeneo ya ubungo wakiwa tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Arusha kumuona mtoto wao kipenzi. Dickson siku hiyo asubuhi aliwahi kazini kwake na kufanya majukumu yake ya kila siku, akiwa ofisini kwake alipigiwa simu na mpenzi wake na kumwambia angelimpitia ofisini baada ya kutoka chuo.
Naam! Johari alikuwa ni moja ya wanafunzi wa chuo kikubwa hapo mkoani, chuo ambacho kilikuwa na wanafunzi wengi wa aina tofauti tofauti, na wengine wakiwa wametokea nchi tofauti tofauti. Ni chuo ambacho kilikuwa kikubwa kutokana na wingi wa wanafunzi waliokuwa wakisoma kwenye hicho chuo. Dickson alikubaliana na mpenzi wake kisha kukata simu na kuendelea na shughuli zake za kila siku.
Johar siku hiyo alipotoka chuoni aliamua kupitia kwa rafiki yake kwenda kumsalimia, alipofika kwa rafiki yake alijikuta amepoteza muda mwingi bila kujua kuwa alisha mwambia mpenzi wake amsubiri. Alipokuja kuangalia saa ilikuwa imeshafika saa kumi kasoro, aliamua kuchukua bodaboda ili kuwahi kwa mpenzi wake.
Wazazi wa Dickson safari yao ilikuwa ndefu lakini Mungu aliwasaidia na walifika salama, walipofika Jijini hapo na muda walijua mwanao angelikuwa ofisini maana ilikuwa bado mapema, waliamua kukubaliana kwenda moja kwa moja ofisini kwa mtoto wao. Johar hakuchukua muda mingi kufika kwa mpenzi wake kutokana na kutumia usafiri, alipofika alimkuta mpenzi wake akiwa anamsubiri huku akionekana kumngoja muda mrefu.
"Baby sorry kwa kuchelewa" Aliongea Johar huku akiwa anampiga busu la mdomoni, Dickson nae alimpa ushirikiano mpenzi wake na kunza kupigana mabusu mazito, maarufu kama denda, ile hali ilichukua kama dakika tano na kuwafanya kila mmoja wao hisia kupanda na kujikuta wakitamani kufanya mapenzi pale ofisini, hisia ziliwazidi na kuwakolea na kujikuta wakianza kufanya mapenzi pale ofisini bila kijali.
Tukija huku kwa wazazi wa Dickson nao walikuwa tayari wamefika ofisini kwa mtoto wao, walipofika waliamua kuingia moja kwa moja ofisini. Walishtuka na kutaka kutudi nje, maana walichokikuta kilikuwa hakielezeki.
ITAENDELEA..........
Picha za mandhari zimetolewa na i-bob. Inaendeshwa na Blogger.