RANGI YA CHUNGWA 2
RANGI YA CHUNGWA 2
WRITER: DEOKING PETER
CONTACT: 0673788242
E-mail: Deokingpeter@gmail.com
FB PAGE: Story Za Deoking
ILIPOISHIA........
Wazazi wa Dickson safari yao ilikuwa ndefu lakini Mungu aliwasaidia na
walifika salama, walipofika Jijini hapo na muda walijua mwanao
angelikuwa ofisini maana ilikuwa bado mapema, waliamua kukubaliana
kwenda moja kwa moja ofisini kwa mtoto wao.
Johar hakuchukua muda mingi
kufika kwa mpenzi wake kutokana na kutumia usafiri, alipofika alimkuta
mpenzi wake akiwa anamsubiri huku akionekana kumngoja muda mrefu.
"Baby sorry kwa kuchelewa" Aliongea Johar huku akiwa anampiga busu la
mdomoni, Dickson nae alimpa ushirikiano mpenzi wake na kunza kupigana
mabusu mazito, maarufu kama denda, ile hali ilichukua kama dakika tano
na kuwafanya kila mmoja wao hisia kupanda na kujikuta wakitamani kufanya
mapenzi pale ofisini, hisia ziliwazidi na kuwakolea na kujikuta
wakianza kufanya mapenzi pale ofisini bila kijali.
Tukija huku
kwa wazazi wa Dickson nao walikuwa tayari wamefika ofisini kwa mtoto
wao, walipofika waliamua kuingia moja kwa moja ofisini. Walishtuka na
kutaka kutudi nje, maana walichokikuta kilikuwa hakielezeki.
ENDELEA.........
Mama yake alipoingia ofisini kwa mtoto wake hakuamini alisho kiona,
alishindwa kuzuia macho yake yasione kilichokuwa kinafanyika, waliamua
kutoka nje kimya kimya bila Dickson kufahamu, maana wakati wanaingia
Dickson hakusikia kitu chchote. Walibaki pale nje ya ofisi ya mtoto wao
kwa dakika kadhaa huku kichwani kwao wakiwa hawaamini kilichotokea,
walihisi pengine siyo mtoto wao wanaemfahamu, maana walijua wazi Dickson
hawezi kufanya ujinga kama ule.
Walikaa kwa muda hatimaye
wakaamua kutoka pale ofisini na kuelekea nyumbani kwa mtoto wao,
hawakutaka mtoto wao ajue kama wazazi wake wameona ujinga aliokuwa
anaufanya. Walipofika nyumbani walimkuta mlinzi wa nyumba ya Dickson,
kwakuwa yule mlinzi aliwatambua kuwa wale ni wazazi wa bosi wake
aliwaruhusu kuingia ndani.
Waliingia ndani huku lile jambo likawa
linawasumbua vichwa vyao, walipofika sebleni hali ilikuwa imebadilika
sana, walikuta baadhi ya nguo zikiwa zimetupwa tupwa kwenye viti vya
kukalia, kitu ambacho kiliwashangaza walikuta hadi nguo za ndani zikiwa
juu ya meza ya pale sebleni. Wazazi hao walibaki wakiwa wanashangaa
njinsi nyumba ya mtoto wao ilivyokuwa chafu hadi kufikia hatua kuleta
kinyaa, walibaki tu wameduwaa walichokifanya wakaamua kutoka na
kumsisitiza kijana wa getini kutimwambia chochote kuhusu ujio wa wazazi
wake pale nyumbani.
Mlinzi huyo hakuwa na kipingamizi zaidi ya
kuwakubalia maana hakuwa anafaha kilichokuwa kinaendelea, alipomaliza
aliwaaga kisha wazazi hao waliondoka na kuelekea nyumba moja kubwa ya
kulala wageni, na kuamua kukaa kwa siku hiyo maana hawakutaka mtoto wao
awaone. Dickson pamoja na mpenzi wake walipomaliza walikubaliana kurudi
nyumbani, huku kula mmoja akiwa anaonekana kuwa na furaha.
Walipofika nyumbani mlinzi wa getini aliwafungulia mlangu wote wakaingia
ndani, mlinzi huyo alionekana kutaka kumwambia bosi wake kama wazazi
walikuja wakati yeye ambapo hakuwepo, likini kutokana na msisitizo wa
wazazi wa Dickson alijikuta analifanya jambo lile siri.
Dickson
pamoja na mpenzi wake waliishi kama watoto wasiojielewa, kama ule
ulikuwa ulimbukeni wa mapenzi basi Dickson pamoja ba Johar mpenzie
walikuwa wamezidi. Kila kitu walichokuwa wanakifanya kilikuwa cha
kitoto, hawakuwa na wanajali chochote zaidi ya kunywa kula na kulala.
Dickson hakuwa yule Dickson aliezoeleka kama Hakimu, hata mlinzi wa
nyumba hiyo alishangaa maisha ya bosi wake yalivyo badilika, alishangaa
kila siku bosi wake alikuwa mtu wa kulewa na kurudi usiku sana tofauti
na hapo awali ambapo hakuwa abatumia kilevi chochote zaidi ya juice na
vinywaji vingine visivyokuwa na kilevi.
Wazazi wa Dickson
walizidi kumfuatilia mtoto wao na kuona mtoto wao alivyo badilika,
walishindwa kuelewa kwanini mtoto wao amebadilika kiasi kile. Hawakupata
jibu la kuwatosheleza zaidi ya wakijiuliza wafanye kitugani ili mtoto
wao kipenzi arudi kama mwanzo.
Waliamua kumfuatilia hatua hadi
hatua, walifanikiwa kumfahamfu msichana aliekuwa akitoka na mtoto wao,
waliamini msichana huyo ndiye aliekuwa akimwaribu mtoto wao.
Walizidi kufatilia na kufahamu msichana huyo alikiwa ni moja ya wanachuo
kikubwa katika jiji hilo, chuo hicho husifika kwa sifa mbaya na
kusemekana baadhi ya wanachuo hicho hujiuza kwa watu wa aina tofauti
tofauti, na wengi wao huathirika kwa ugonjwa wa ukimwi.
Walijikuta wakipata mawazo mengi juu ya mtoto wao kipenzi, walijaribu
kutafuta watu wa kuwasaidia lakini hawakufanikiwa zaidi ya kuzidi kuumia
kwa mawazo.
Dickson alizidi kula rahaa na mpenzi wake huku akiwa
hatambui kama familia yake ilikuwa pale mkoana, na kibaya zaidi familia
yake walikwisha kugundua ujinga aliokuwa akiufanya.
ITAENDELEA...............