Baraka da Prince akasirishwa kuona Linex kasema amefanya upuuzi kusambaza video ya Mwanamke Whatsapp
Kupitia kwa Soudy Brown kwenye YOU HEARD ya CloudsFM, mwimbaji staa wa bongofleva Linex alihojiwa kuhusu ishu inayoendelea kwenye mtandao wa Whatsapp ya kusambazwa kwa video ya mpenzi mpya wa Linex akionekana mapenzini kitandani na mwimbaji Baraka Da Prince ambaye anatajwa kuwa mpenzi wake wa zamani hivyo Baraka anatuhumiwa kuisambaza hiyo video.
Baada ya hii ishu kumfikia Baraka, ameongea kwenye Exclusive na AyoTV na kusema ‘Sijawahi kutembea na mtu ambaye katembea na Linex…. kwanza hawezi kutembea na mtu ambaye mimi natembea nae, yeye labda ndio anataka hiyo kiki ila mimi siwezi kutaka kiki kwa Linex, Linex kanikosea‘