Baada ya Q. CHILLAR kusema DIRECTORS wa ndani hawana uwezo wa kufanya nao kazi, Dir HANSCANA kamjibu
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo
kinachorushwa na East Africa Radio, Hanscana amesema Q Chief ana stress
za maisha, kwani kwa muda mrefu yupo kwenye game na ameshindwa kufanya
chochote.
“Ye ana stress za maisha, haiwezekani
ukafanya muziki zaidi ya miaka 17 alafu huna hata pikipiki wakati kuna
watoto wamekuja tu juzi kirahisi rahisi, mtu sijui anaitwa Baraka da
Prince kwa hiyo lazima upate mastress uanze kutapatapa, si unajua mfa
maji, u can see ur self jamaa ana more than 17 yrs in the game alafu he
got nothing, alafu kuna watoto tu wadogo wanafanya kitu, kwa hiyo
unaweza ukafikiria, suala dogo kama hilo kitaalamu hizo ni stress za
maish”. Alisema Hanscana.
Pamoja na hayo Hanscana amemtaka Q Chief
akae pembeni na kuwaachia wasanii wachanga wafanye kazi kwa sasa, na
yeye abaki kuwa mtazamaji.
“Ninachomshauri atuachie tu new
generation tufanye vitu vyetu , tuna mwaka mmoja ndani ya game tuna
drive, tunaishi vizuri, atuache tu vijana aangalie tu game awe
anatuangalia Youtube”, alisema Hanscana.
hapo jana msanii Q Chief alisema
directors wa ndani hawana uwezo wa kufanya nao kazi, na kuwataka
wakaongeze taaluma zaidi ili kuweza kufanya vizuri.
Source: http://www.eatv.tv/